SIGN THE DECLARATIONKiswahili

Azimio la Washington D.C.

KUGEUZA MKONDO PAMOJA:

ILANI YA KUANGAMIZA JANGA LA UKIMWI

Tuko katika wakati wa kipekee katika historia ya jaNga la UKIMWI.

Miongo mitatu ya upiganiaji, utafiti, na utoaji wa huduma stahimilivu kwa jamii imeifikisha dunia katika hali ambayo haikuwazika miaka michache mifupi iliyopita: uwezekano wa kuanza kuangamiza janga la UKIMWI wakati wetu. Hasara imekuwa ya kutohesabika; faida za ajabu. Lakini sasa, kupitia maendeleo mapya ya kisayansi, na ushindi wa jamii, siasa na haki za binadamu, tumegundua kwamba inawezekana kukusanya na kuwasilisha jumla ya mbinu zilizothibitishwa, ambazo, kama zitatekelezwa ipasavyo, zinaweza kugeuza mkondo wa UKIMWI.

Bado tunahitaji dawa ya kuponya na dawa ya chanjo. Lakini lazima tuongeze rasilimali na bidii yetu kwa kutumia vifaa tulivyo navyo leo kuzuia maambukizo mapya na kuboresha afya ya mamilioni ya watu walio na VVU/UKIMWI. Mamilioni ya maisha yataokolewa.

Kugeuza mkondo dhidi ya janga la VVU/UKIMWI kutachukua uongozi wa pamoja katika ngazi zote za serikali, mifumo ya afya, masomo na mashirikia yasoi ya kiserikali. Lazima tujitahidi kwa mitazamo ya nidhamu mbalimbali inayoheshimu na kutetea haki za binadamu na hadhi ya watu wote walioathiriwa na janga hili. Lengo la kuanza kuangamiza janga la UKIMWI ni la nia ya juu, lakini linaweza kutimizwa. Liko katika uwezo wetu.

saini Azimio

Ili tugeuze mkondo huu pamoja lazima:

 1. Tuongeze uwekezaji mpya. Tunaweza kuokoa maisha, kuzuia maambukizo na kupunguza bei ya janga duniani kwa kuongeza uwekezaji muhimu kwa haraka. Maendeleo makubwa zaidi yatahitaji ahadi za fedha za kipimo kilicho sawa kutoka kwa wafadhili kote duniani na ndani, ikiwa ni pamoja na kutoka kwa serikali za kitaifa duniani kote.
 2. Tuhakikishe kinga, matibabu na matunzo ya UKIMWI yenye ushahidi kwa kukubaliana na haki za binadamu za wale walio katika hatari kubwa na walio na mahitaji zaidi. Hii ni pamoja na wanaume wanaofanya mapenzi na wanaume wenzao, watu wasenge, watu wanaotumia madawa ya kulevya, wanawake waliohatarini, vijana, wajawazito wanaoishi na VVU, na makahaba, na pia watu wengine walioathiriwa. Hakuna mtu anapaswa kutengwa ikiwa tunapanga kufikia lengo letu.
 3. Tuangamize unyanyapaa, ubaguzi, vikwazo vya kisheria na unyanyasaji wa haki za binadamu dhidi ya watu wanaoishi na VVU na wale walio hatarini. Unyanyapaa na ubaguzi unazuia juhudi zetu zote na kuzuia utoaji wa huduma muhimu.
 4. Tuongeze kwa dhahiri upimwaji wa VVU, utoaji ushauri na uhusiano wa kinga, huduma za kuponya na usaidizi. Kila mtu ako na haki ya kujua hali yake ya VVU na kupata matibabu, dawa na usaidizi wanaohitaji
 1. Tutoe matibabu kwa wanawake wote wajawazito na wanaonyonyesha wanaoishi na VVU na kuangamiza uambukizaji wakati wa kujifungua:
  Tunaweza kusaidia wanawake waishi na wawe na afya nzuri na tuangamize maradhi ya VVU kwa watoto wachanga
 2. Tuongeze ufikio wa matibabu ya kupunguza makali ya VVU/UKIMWI kwa wote wanaohitaji. Hatuwezi kuangamiza UKIMWI mpaka ahadi ya ufikio ulimwenguni itimizwe
 3. Tutambue, tubainishe na tutibu kifua kikuu (TB). Tutekeleze mipango ya kuzuia kifua kikuu kupitia huduma za VVU na kifua kikuu zilizounganishwa. Hakuna tena kuishi na VVU lakini kuuawa na kifua kikuu.
 4. Tuharakishe utafiti kuhusu vifaa vipya vya kukinga na kutibu VVU, ikiwa ni pamoja na njia mpya kama vile tiba ya kuzuia maradha kabla ya kuambukizwa (PrEP) na vizuizi vya vijiumbe maradhi, na utoaji bora wa kile tunachojua kinafanya kazi ipasavyo, kuanzia kondomu mpaka matibabu kama kinga. Tuongeze utafiti wa dawa ya chanjo na dawa ya kuponya. Utafiti ni muhimu kwa kutusaidia kupigana na janga hili.
 5. Tuhamasishe na uhusishaji muhimu wa jamii zilizoathiriwa lazima uwe katika kiini cha mikarara ya pamoja. Uongozi wa wale walioathiriwa moja kwa moja ni muhimu sana kwa mkarara unaofaa wa VVU/UKIMWI

 

Changamoto zilizo mbele ni kubwa, lakini hasara ya kutofaulu itakuwa kubwa zaidi. Tunawaomba watu wote wanaojali wa jamii ya duniani, katika moyo wa mshikamano na utekelezaji wa umoja, na kuishughulisha kabisa jamii ya watu wanaoishi na VVU, kutafuta umuhimu mpya wa kupanua vita duniani dhidi ya UKIMWI. Lazima tuchukue hatua kwa yale tunayoyajua. Lazima tuanze kuangamiza UKIMWI – Pamoja

download Azimio